KING FM RADIO 2017
104.3
Banner 3
Banner 2

Welcome to Kings FM

About Kings

Kings FM is a privately owned radio station wholly owned by Kings Broadcasting Service Limited. The company was conceptualised in 2007, but officially started in 2010. The company was established with the principal objectives of providing professional broadcasting services. Kings FM Radio went on air on 13th June 2014 through 104.1 Mhz FM (Stereo) Covering about 94% of Njombe region area. The full programming started officially.

Read More 

Latest News

 • News

  • MASHIRIKA YA KIRAIA KUOMBA GRACE MUGABE AONDOLEWE KINGA.
   2017-08-22 06:34:58

   MASHIRIKA YA KIRAIA KUOMBA GRACE MUGABE AONDOLEWE KINGA.Shirika la wanaharakati nchini Afrika Kusini, Afriforum, limetangaza Jumatatu hii Agosti 2 nia yake ya kuwasilisha maombi yake mbele ya mahakama ya kutaka mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aondolewe kinga ya kidiplomasia iliyotolewa na serikali ya Afrika Kusini. Grace Mugabe anashtumiwa kumshambulia Gabriella Engels mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. "Tutaomba mahakama kusema kwamba uamuzi wa wa kumpa mkewe rais `mugabe kinga ya kidiplomasia ni kinyume cha sheria kwa sababu,...

  • DONALD TRUMP KUKUTANA NA VLADIMIR PUTIN WIKI IJAYO.
   2017-06-30 10:36:09

   DONALD TRUMP KUKUTANA NA VLADIMIR PUTIN WIKI IJAYO.Ikulu ya White House yathibitisha uwepo wa mkutano kati ya Donald Trump na Vladimiri Putin wiki ijayo Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani. Mkutano wa viongozi hawa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20). Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado haijafahamika mada maalumu itakayozungumziwa katika mkutano wa wawili hao. Mapema wiki hii ikulu ya...

  • UJERUMANI KUHARARISHA NDOA ZA MASHOGA.
   2017-06-30 10:34:09

   UJERUMANI KUHARARISHA NDOA ZA MASHOGA.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihojiwa maswali Bungeni. Ujerumani inatazamiwa kujiunga Ijumaa hii na nchi nyingi za Magharibi kwa kuhalalisha kupitia kura za wabunge ndoa ya mashoga, baada ya Angela Merkel kuachana na upinzani wake wa maadili chini ya shinikizo la maoni ya umma. Angela Merkel angependelea kura hiyo ipigwe baada na bunge lijalo, baada ya uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa mwezi Septemba, wakati wa chama chake cha kihafidhina, kilichogawanika kuhusu suala hilo, kuweza...

  • MTU ALIYEJARIBU KUSHAMBULIA MSIKITI AKAMATWA PARIS.
   2017-06-30 10:31:50

   MTU ALIYEJARIBU KUSHAMBULIA MSIKITI AKAMATWA PARIS.Polisi ya Ufaransa imefaulu kumkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja nchini humo. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mtu huyo alikua na lengo la kuua kwa makusudi. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mtu huyo alikua na lengo la kuua kwa makusudi. Polisi inasema kwamba inaendelea kumshikilia mtu huyo, na tayari uchunguzi umeanzishwa ili kujua kwamba alishirikiana na watu wengine katika kitendo hicho. Pia polisi...

  • SERIKALI YA BURUNDI YAMUONYA MJUMBE MAALUM WA UMOJA WA MATAIFA
   2017-06-30 10:29:49

   SERIKALI YA BURUNDI YAMUONYA MJUMBE MAALUM WA UMOJA WA MATAIFAMjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Burundi rais wa zamani wa BurkinaFaso Michel Kafando, amemaliza zaira yake Alhamisi Juni 29 ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteueliwa kwake, ambapo baadae atatembelea katika nji jirani kukutana na mratibu katika mazungumzo ya warundi, Bejamini William Mkapa, kisha ataelekea nchini Uganda kukutana na msuluhishi Yoweri Kaguta museveni kabla ya kuhitimisha ziara yake katika makao makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Abeba nchini Ethiopia. Ni...

  • SHERIA YA TRUMP KUHUSU UHAMIAJA YAANZA KUTUMIKA.
   2017-06-30 10:26:00

   SHERIA YA TRUMP KUHUSU UHAMIAJA YAANZA KUTUMIKA.Sheria ya rais wa Marekani kuhusu uhamiaji na usafiri kwenda Marekani kwa raia kutoka nchi sita za Kiislamu imeanza kutekelezwa leo Ijumaa saa sita usiku (00:00). Kwa sasa raia kutoka mataifa hayo sita ya Kiislamu na wakimbizi wote wanakabiliwa na masharti magumu ya kuingia nchini Marekani. Kulinagana na sheria hii mpya ya usafiri nchini Marekani, Bibi, shangazi, mjomba, binamu na mpwa hawakubaliki kuwa watu wenye uhusiano wa karibu na mtu anayetaka kuingia taifa hilo. Sheria hii inamaanisha kwamba...

  • RAIS TRUMP ACHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA KUZUIA HAKI.
   2017-06-15 10:30:37

   RAIS TRUMP ACHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA KUZUIA HAKI.Vyombo vya Habari nchini Marekani vinaripoti kuwa rais Donald Trump anachunguzwa na wakili maalum Robert Mueller kwa tuhma za kuzuia haki. Maafisa wa juu wa Inteljensia nchini humo wanatarajiwa kuhojiwa kufahamu ukweli uliomfanya rais Trump kuagiza kusitishwa kwa uchunguzi wa aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn. Washauri wa rais Trump wamesema wameshangazwa sana na kuvuja kwa kinachoendelea kwa vyombo vya Habari. Ripoti ya uchunguzi huu imechapishwa katika magazeti ya...

  • WATU 19 WAUAWA MJINI MOGADISHU BAADA YA KUSHAMBULIWA NA AL SHABAB.
   2017-06-15 10:16:54

   WATU 19 WAUAWA MJINI MOGADISHU BAADA YA KUSHAMBULIWA NA AL SHABAB.Watu 19 wameuawa baada ya kundi la kigaidi la Al Shabab kutekeleza shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia. Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilenga mkahawa maarufu katika mji huo mkuu. Gari dogo lililokuwa limetegwa bomu lilipuka lakini pia magaidi hao kuwapiga risasi baadhi ya watu waliokuwa ndani ya mkahawa huo. Abdi Bashir afisa wa usalama nchini humo amesema magaidi hao watano waliwazuia watu ndani na Mkahawa huo na kuanza kuwapiga risasi lakini wakalemewa. Aidha amesema...

  • JOSEPH KABILA: SIJAWAHI KUAHIDI KUANDAA UCHAGUZI DRC CONGO
   2017-06-05 07:22:01

   JOSEPH KABILA: SIJAWAHI KUAHIDI KUANDAA UCHAGUZI DRC CONGORais wa Jamhuri ya Kidemokradia ya Congo, Joseph Kabila Kabange amesema hajawahi kuahidi kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini mwake mwaka huu.   Kabila ameliambia Jarida la kila wiki la Ujerumani la Der Spiegel kuwa hajaahidi chochote lakini anapenda Uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.   Aidha, amesema anataka uchaguzi mzuri lakini sio tu kufanya uchaguzi.   Hayo yanajiri wakati ambapo joto la kisiasa kuhuu uchaguzi kufanyika mwaka huu nchini DR Congo imeendelea kupanda, huku upinzani hasa ule...

  • FAURE GNASSINGBE ACHAGULIWA KUWA RAIS WA ECOWAS
   2017-06-05 06:58:07

   FAURE GNASSINGBE ACHAGULIWA KUWA RAIS WA ECOWASRais wa Togo Faure Gnassingbé ndiye rais wa sasa wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi Afrika Magharibi ECOWAS. Alichaguliwa siku ya Jumapili Juni 4 katika mkutano wa 51 wa viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS mjini Monrovia, nchini Liberia. Anachukuwa nafasi ya rais wa Liberia Ellen Johanson Sirleaf   Faure NGnasingbe alitoa wito kwa ushirikiano zaidi na kupongeza maendeleo ya kiuchumi yaliofikiwa katika ukanda huo wa Afrika Magharibi, wakati ambapo moja ya maamuzi ya mkutano huo ni kujenga barabara kuu...

  • MFALME WA MOROCCO AGOMA HUDHURIA MKUTANO WA ECOWAS
   2017-06-05 06:28:44

   MFALME WA MOROCCO AGOMA HUDHURIA MKUTANO WA ECOWASMfalme wa Moroco ameahirisha kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya mataifa ya Afrika magharibi huko Liberia kufuatia uwepo wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Nyatanyahu,wizara ya mambo ya kigeni imearifu.   Taifa hilo la afrika kaskazini lina matumaini ya kujiunga katika jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS baada ya umoja wa Afrika kuirejesha nchi hiyo ya Morroco tangu ilipojitoa miaka 33 iliyopita.   Mfalme Mohamed VI alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa ECOWAS mjini Monrovia jumamosi na...

  • NCHI 4 ZA KIARABU ZAVUNJA UHUSIANO WAO NA QATAR
   2017-06-05 06:26:16

   NCHI 4 ZA KIARABU ZAVUNJA UHUSIANO WAO NA QATARNchi nne za Kiarabu ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Bahrain na Umoja wa Nchi za Kiarabu wamevunja uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi ya Qatar wakiisishtumu kuhusika au kuchangia kwa njia moja ama nyinge kwa kuvuruga ukanda huo.   Nchi hizi nne zimeishtumu Qatar kuunga mkono na kusaidia ugaidi. Qatar imelaumiwa kusaidia na kuunga mkono kundi la Muslim Brotherhood, lililopigwa marifuku nchini Misri.   Shirila la taifa la habari nchini Bahrain limesema kuwa nchi hiyo inavunja uhusiano wake na...

  • IS YADAI KUHUSIKA NA SHAMBULIO LA LONDON
   2017-06-05 06:23:50

   IS YADAI KUHUSIKA NA SHAMBULIO LA LONDON  Polisi ya Uingereza imeendelea na msako hadi usiku wa manane katika eneo maarufu la Barking mashaiki mwa mji wa London, ambapo watu kadhaa walikamatwa. Kundi la Islamic State lilikiri siku ya Jumap[ili kwamba lilihusika na shambulio hilo.   Katika taarifa mpya, mkuu wakikosi cha kukabiliana na ugaidi alisema kwamba wachunguzi wamekua wakiendelea na kazi yao na wametambua watu walilioendesha shambulio dhidi ya mji wa London siku ya Jumamosi usiku.   Polisi kwa sasa inachunguza kama watu hao...

  • TAZAMA VIDEO MPYA YA DAVIDO - FALL (OFFICIAL VIDEO)
   2017-06-02 15:13:57

   TAZAMA VIDEO MPYA YA DAVIDO - FALL (OFFICIAL VIDEO)  Baada ya Kufanya vizuri na wimbo wake wa IF uliomrudisha vizuri kwenye muziki baada ya kutofanya vizuri kwa muda, Mwanamuziki Davido ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la FALL.   

  • HALI YA HEWA: JUMUIYA YA KIMATAIFA YAPINGA UAMUZI WA TRUMP
   2017-06-02 15:04:16

   HALI YA HEWA: JUMUIYA YA KIMATAIFA YAPINGA UAMUZI WA TRUMPViongozi mbalimbali wa dunia wamekerwa na hatua ya rais Trump kuiondoa Marekani katika mkataba huo uliotiliwa saini na mataifa 187 jijini Paris, nchini Ufaransa mwaka 2015. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani hatua hiyo ya rais Trump na kusisitiza kuwa Ufaransa itatekeleza mkataba huo ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha amesema, utekelezwaji wake ni muhimu kwa manufaa ya dunia katika siku zijazo. China imesema hatua ya Marekani inarejesha nyuma juhudi za...

  << < 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 > >>

Our Facebook Page

Call us:
(+255) 026-2782454
Address:
P.O.Box 1086, Chaungingi ST, Njombe, Tanzania.
Telephone: (+255) 026-2782454
E-mail: info@kingsfm.co.tz
Location      Contact Us